Saturday, 4 June 2016

David de Gea aweka wazi nini anakitaka sasa Manchester United chini ya Mourinho

David de Gea amesisitiza kwamba anataka kushinda “mataji mengi zaidi” katika Manchester United chini ya utawala wa meneja Jose Mourinho, baada ya kuwa na utendaji bora katika misimu miwili  chini ya ukufunzi wa Louis van Gaal, ripoti kutoka Sportsmole.

Mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikuwa karibu kujiunga na Real Madrid kiangazi kipitacho lakini mwishowe alisaini mkataba mpya na United, alisemwa kuwa anaweza kujiunga na Santiago Bernabeu katika miezi ifuatayo.

“Kuongea kuhusu Jose Mourinhoni kuongea kuhusu ushindi. Ushindi ni wa United, ni wa Jose na falsafa yangu. Tunaweza kufanya timu kubwa na namkaribisha vizuri. Nilisaini mkataba wa miaka mitatu mingine na United na nataka kushinda mataji mengi hapa,” DeGea aliiambia Marca.