Thursday, 26 May 2016

Shilole na Vanessa wapanga kumaliza vita yao kwa hii staili ya pekee

Hivi karibuni kumekuwa na vita ya maneno baina ya madiva wawili wanaotamaba katika muziki wa Bongo kwa sasa.

Shishi na Vanessa Mdee wamekuwa wakirushiana sana maneno ya vitisho huko kwenye mitandao ya kijamii ambapo kila mmoja akijaribu kurusha kombora zitakazo muumize mwingine.

Sasa haya maneno yamefika mwisho sasa maana wahenga wanasema maneno tupu hayavunji mfupa.

Shishi na Vee money watapanda jukwaani siku ya Jumapili tarehe 29 May pale Club Billcanas kupambana kimuziki na hapo ndipo atakapoonekana nani mbabe.

Lakini hawa wote yaani Shishi na Vee bado wanatambiana hata kabla ya shoo kufanyika. Huko Insta wameyaandika haya,

Vanessa ameandika; Talk is cheap. Tukutane Bilicanas. Umeongea sana. Tukutane jukwani Jumapili huku Shilole akijibu:  Veee are u sure????