Nyota matata wa klabu ya Leicester city Jamie Vardy atakosa mechi ya kirafiki kati ya timu yake ya taifa England na Australia kwa sababu anatarajia kufunga pingu za maisha siku mbili kabla ya mchezo huo.
"Vardy anastahili apate mda ili aweze kufunga ndoa yake," Roy Hodgson, kocha timu ya taifa England aliweka wazi.
Vardy ambaye amepewa muda wa kufanya ndoa yake amedai kuwa atarudi tena mazoezini baada ya mambo ya ndoa kupita na kuitumikia timu yake ya taifa.