Meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kama meneja mpya wa Manchester United.
Meneja Mreno, ambaye alikuwa katika
mazungumzo na Red Devils tangu Jumanne, anakalia kiti cha Louis van Gaal aliyefutwa kazi Jumatatu asubuhi.
Kwa mujibu wa Sky Sports , Mourinho amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £45m na tangazo rasmi kwenye tovuti rasmi ya klabu latarajiwa kutangazwa hivi punde kabla
ya wikendi.
Jose Mourinho alikuwa anakaa bila kazi tangu afukuzwe na Chelsea Disemba mwaka jana.