Tuesday, 24 May 2016

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine

May 23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaJohn Pombe Magufuliamefanya uteuzi wa viongoziwawili wa serikali, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi BaloziJohn Kijazileo imeeleza kuwa Rais waMagufuliamemteua Gerson J. Mdemukuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya Uteuzi huo,  Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk), Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi. Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na uteuzi huu umeanza mara moja.

Millardayo.com