Monday, 23 May 2016

Adele kusaini label ya Alikiba Sony Music kwa dau la Paundi milioni 90

Adele anatarajia kuwa msanii mpya wa record label ya Sony Music, iliyomsainisha Alikiba wiki iliyopita.

Imeripotiwa kuwa msanii huyo atasaini mkataba wenye dau la paundi milioni 90, kubwa zaidi kwa msanii wa Uingereza. Kama ni kweli, kiasi hicho kitaongeza utajiri wake mara mbili ambao kwa sasa ni £85m.

Mkataba huo utakuwa mkubwa zaidi kwa mwanamuziki wa kike kwenye historia ya muziki. Mkataba wake na label ya mwanzo XL umemalizika

Bongo5.com