Raymond amefafanua kinachoendelea kati yake na Harmonize kutokana na maneno yaliyoanza kuzungumzwa mtaani kuwa Harmonize ameanza kumkunjia Raymond.
Raymond kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake‘Natafuta Kiki’kwenye redio na mtaani japo hauna muda mrefu tangu auachie.
Akiongea kwenye kipindi cha 5 Selekt, kinachoruka kupitia EATV, Raymond alisema yeye na Harmonize hawana tatizo lolote na kila mtu anafanya muziki wake.
“Harmonize anafanya muziki mzuri, mimi hiyvo najitahidi kidogo watu wanasema nafanya vizuri. Lakini wotetunafanya muziki, Harmonize ana nyimbo zake nyingi nzuri ambazo nazijua ambazo najua watu hawazijui,” alisema.
Bongo5.com