Maelfu ya watu nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi dunianiya Antonov An-225 Mriya, ilipowasilimjini Perth nchini humo.
Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.
Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha masharikiya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.
Bbcswahili