Monday, 16 May 2016

Pelle asema Messi si mfalme wa soka wa Argentina na kumtaja huyu ndiye mfalme wao

​Lionel Messi si mchezaji bora wa Argentina wa muda wote, Gwiji wa Brazili anaamini nyota huyo wa Barcelona ni wa pili nyuma ya gwiji la Real Madrid Alfredo Di StefanoLicha ya kumweka wa pili baada ya Di Stefano, Pele amesema Messi ni “Mwana wa Mfalme” tu kwa sababu mfalme ni yeye mwenyewe hadi sasa katika soka.

Maneno hayo ya Pele yamekuja baadaya Barcelona anayocheza Messi kutwaa taji la sita La Liga katika kipindi cha miaka nane hali kadhalika mataji matatu ya Ligi ya Mabinhwa Ulaya katika kipindi hicho.

“Iwapo mimi ni Mfalme, Basi Messi atakuwa mwana wa Mfalme kwa kipindi cha miaka 15,” Pele alikiambia La Vanguardia kupitia Goal.

“Siwezi kumuita Mfalme, kwa sababu mfalme ni mmoja tu. Naamini kwamba Alfredo Si Stefano alkuwa mchezaji aliyekamilika kuliko nyota wote wa Argentina, alikuwa kamili kuliko Diego Maradona na Messi.

“Nafurahi kwamba nilicheza katika enzi zanfu, pamoja na ukweli kwamba mambo ni marahisi zaidi sasa.“Wachezaji kama Di Stefano na Mimi hawawezi kujulikana sana kwa sababu teknolojia ya kurekodi ilikuwa duni."

Miamba wa Catalan wamepewa makali na Messi, na Hat-trik ya Luis Suarez ikawazamisha Granada bao 3-0 na kuwawezesha Barcelona kutwaa ubingwa La Liga.

Pamoja na kupata msaada mkubwa kutoka kwa Suarez na Neymar msimu huu, Mwargentina huyo bado alifanikiwa kufunga mabao 26 na kutoa pasi 16 za magoli katika kampeni za La Liga.Messi amekiri kwamba atakuwa tayarikuiwakilisha Argentina katika michuano ya Copa America majira ya joto, itakayofanyika Marekani, na ni mara ya kwanza michuano hii kuandaliwa nje ya bara la Amerika Kusini.

Goal.com