Friday, 27 May 2016

Mourinho asaini mkataba wa miaka 3 Manchester United

Jose Mourinho ametangaza rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United.

Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.

Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la Dunia.

"José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa," naibumwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.

Mourinho, 53, amesema: "Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa sana katika mchezohuu. Ni klabu inayofahamika sana na kuenziwa kote duniani.”

Amesema amekuwa akihisi mvuto wa kutaka kuwa Old Trafford na kwamba daima amekuwa akisikizana na mashabiki wa United.

“Nasubiri kwa hamu kuwa meneja wao na kujivunia uungwaji mkono wao miaka ijayo.

“Kuna hisia fulani na upendo ambaohuwezi kupata kutoka kwa klabu nyingine."

Mourinho amekuwa bila kazi tanguafutwe na klabu ya Chelsea Desembamwaka jana.Mourinho ametia saini mkataba baada yamazungumzo ya siku tatubaina yake, wakala wake Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United.Moja ya mambo ambayo anatarajiwa kuyafanya ni kumchukua mshambuliaji kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic, ambayewalifanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan.

Bbcswahili