Mwanamitindo ambaye ni meneja wa Diva wa filamu za Kitanzania, Wema Sepetu, Martin Kadinda, amekiri kuwa mrembo huyo ni pasua kichwa kwa kuwa ni ngumu kubadilisha misimamo yake kama hujamzoea.
Akizungumza na Papaso la Burudani hivi karibuni alipotembelea ofisi za gazeti hili, Martin alisema kabla hajaamua kuanza kufanya kazi na Wema, ilimbidi achukue muda ili ajenge urafiki utakaomsaidia kufanya kazi zake za kimeneja bila shidayoyote.
“Kitu ambacho kinatusaidia tunafanya kazi bila tatizo ni urafiki wetu wa muda mrefu ulioanza kabla sijawameneja wake.Wema ni mtu ambaye usipomzoea atakusumbua, hapendi kubadilisha msimamo wake kirahisi,” alisema martin.
Bingwa Newspaper