Sunday, 22 May 2016

Kumbe kuna wabunge wavuta bangi na wala unga? Spika wa Bunge awafichua wabunge wala unga na bangi

KAMA unashangaa kusikia kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ametimuliwa kwa kuingia bungeni akiwa amelewa.

Bila shaka utachoka zaidi ukisikia kuna wabunge kadhaa huingia kwenyeukumbi wa Bunge wakiwa wametumiavilevi vikali zaidi vikiwamo bangi, viroba na dawa za kulevya.Spika wa Bunge, Job Ndugai, ndiye aliyefichua siri hiyo jana wakati akizungumza na Nipashe juu ya hatuaya Rais John Magufuli kumtimua Kitwanga katika Baraza lake la Mawaziri kwa sababu aliingia bungenina kujibu swali la wizara yake akiwa amelewa.

Kutokana na hali hiyo, Ndugai alisemasasa wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa ushauri nasaha watakaowapa msaada wa kisaikolojia.

“Kikubwa tunataka kuweka mkakati wa kujaribu kumtambua (mbunge) mmoja mmoja na kujaribu kuwatafutawale watu wanaotoa ushauri nasaha au watu wa mambo ya saikolojia.

“Tunajaribu ku-identify (kuwatambua) watu maalum wanaoweza kutusaidia kuzungumza na hawa watu ili waondokane na matatizo yale ambayotutaweza kuyagundua… lakini wale wanaofanya kwa kificho itakuwa tabu kidogo. Lakini huko mbele tutakwendakwenye vifaa,” alisema Ndugai na kuongeza:

“Maana siyo ulevi tu, kuna sigara kubwa (bangi), unga (dawa za kulevya)… watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi,” alisema Ndugai.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa kwa taarifa hiyo asieleweke vibaya kuwa niwabunge wote hutumia vilevi kabla ya kuingia bungeni, bali wapo wachache wenye kawaida hiyo na kwamba hao ndiyo wanaostahili kusaidiwa na wataalamu wa saikolojia na pia kufunga vifaa maalum vya kuwabaini.

“Simaanishi wote (wabunge), maana mtu anaweza kufikiri ni wabunge wote… hapana. Hili ni kundi dogo mno la wabunge (na) hawajai hata mkononi. Lakini wabunge walio wengi ndiyo wazuri sana, hawanywi pombe wala nini. Kikundi hiki kinahitaji msaada wa ushauri,” alisema.