Uhusiano wa Drake na Rihanna uliokuwa umepamba moto ndani ya wiki mbili zilizopita sasa umeingia doa.
Imeripotiwa kuwa wapenzi hao wametengana kwa kile kinachodaiwa kuwa Rihanna alifumwa na Drake akizungumza na Chris kupitia simu na hii inamaanisha wawili hao bado walikuwa pamoja.
Kama hiyo haitoshi Drake alishawahi kuzikuta meseji za Chris Brown kwenye simu ya Rihanna jambo lililomkasirisha sana Drake na kuamua kufunga vioo, vyanzo vilisema.
Inasemekana kwamba Chris na Rihanna walishafanya mipango ya kuridiana tena.
Itakumbukwa kuwa Chris ameachwa na Karrueche siku kadhaa zilizopita, sasa hii inaaemwa kuwa Karrueche alimwacha jamaa kisa alizikuta meseji za Rihanna kwenye simu.