Saturday, 29 March 2014

Picha za ndoa ya kwanza ya mashoga kufungwa Uingereza, watu waishangilia ile mbaya. Hebu twende na vitendo hapa.

Kweli msemo wa mimi cha nini mwenzio anajiuliza atakipata lini unasadifu haya yanayotokea hapa dunia.

Wakati Uganda ikiwa ina sheria kali ya kuzuia ushoga, mambo ni tofauti huko Uingereza na Wales ambako leo mapena asubuhi watu walikusanyika kushangilia ndoa ya kwanza ya jinsia moja kufungwa nchini humo.

Kusherehekea huko kulikuja baada ya sheria inayoruhusu ndoa za aina hiyo huko Uingereza na Wales kuhalalishwa ufanyaji kazi wake usiku wa manane.