Ukiachana na kukuzaa, mama ana mengi aliyoyafanya kwako hadi sasa umefikia kwenye hatua hiyo uliyonayo. Ni mtu wa pekee sana katika maisha yako na ni mtu anayehitaji heshima ya kipekee mno.
Hivyo basi, una vitu vingi ambavyo unavyo kwa sasa ambavyo unahitaji kumshukuru mama;
Mshukuru kwa tabia yako uliyonayo, inaaminika kwamba tabia ya mtoto uchangiwa na mama kuwa jinsi ilivyo, hivyo basi tabia yako nzuri uliyonayo ni matunda mazuri ya malezi bora ya mama. Anastahili hongera kwa hili.
Mshukuru kwa kukukumbusha na kukusisitiza kwenda shule. Kama ilivyosemwa hapo mwanzo ni mama anayejenga mazingira fulani ya mtoto na ni yeye aliyekuwa anakuhimiza kwenda shule kila siku na ndio maana leo hii unajua kusoma na kuandika. Wapo watoto ambao mama zao hawawajali hata kidogo, hivyo basi, kwa hili, mama anastahili shukrani.
Kukufulia nguo zako, kukuogesha ni jambo lingine unalohitaji kumshukuru mama. Ni kazi kubwa sana aliyoifanya mama ambayo inahitaji uvumilivu sana. Kukufulia nguo zako na kukufanya ujiite msafi leo hii ni matokeo ya mama kukufulia na kukuogeasha. Kwa hili mpe shukrani mama.
Mshukuru kwa kuwa msaada wa kwanza pale ulipopata tatizo. Kwenye hatua ya utoto huwa mtoto anakumbana na matatizo lukuki ambayo mama peke yake ndiye msaada namba moja. Kwa hili, mshukuru yeye.
Mama amekuwa akifanya kazi kubwa sana na ya kuchosha ya kukubembeleza unyamaze kulia. Ni jambo la kushukuru mama kwa upendo wake huo wa kukupoza.
Mshukuru mama kwa kukufanya huwe na afya njema leo hii kwa kukupa vyakula vyenye virutubisho ikiwemo maziwa yake. Ni bahati sana kwa watoto wengine kuonja ziwa la mama. Wewe uliyepata ziwa la mama na kujenga afya ulionayo sasa mshukuru mama.
Kwa nini usimpe hongera yake sasa, hebu mwambie mama hongera mama.