Wednesday, 26 March 2014

Kumbe kuna biashara ya kusafirisha watoto wa kike kwenda China kufanya ukahaba!? Ebu twende hapa na vitendo tufuatilie hili.

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa kusababisha kunyanyaswa kwa
wasichana hao na wengine kuuawa.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema
serikali itatuma wachunguzi nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.

Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini China.

Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wadogo kwa kisingizio
cha kuwatafutia ajira.

Baadhi ya wanaosafirishwa hujikuta pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa kushiriki ukahaba.

Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam
waliozungumzia tatizo hilo na wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali ichukue hatua.