Gazeti la De Morgen la nchini Ubelgiji lipo matatani kwa sasa likiwa linakabiliwa na mashitaka ya kuonyesha itikadi ya ubaguzi wa rangi juu ya picha hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti lao.
Maelezo toka gazeti hilo yanasema picha hiyo ilichapishwa kama sehemu ya maoni ya mhariri. Pia ililipotiwa kuwa, baadae gazeti hilo lilichapisha maelezo ya kuomba msamaha kwa kukubali kuwa limefanya makosa.