Monday, 24 February 2014

Taarifa zaidi kuhusu Rais wa Uganda kutia saini sheria ya kuzuia ushoga.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki
mapenzi ya jinsia moja.

Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi
wa habari.

Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza, adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.

Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale
wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi. 

Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.

Kwenye picha ni kijana anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

BBC swahili