Raisi wa Marekani Barack Obama amesema kwamba, amesikitishwa na mbio za Uganda kuelekea upitishaji wa sheria ya kuzuia ushoga nchini humo.
Obama aliyazungumza hayo jumapili na kusema kuwa sheria za kuzuia ushoga ni hatua ya kuyarudisha nyuma mataifa ya Afrika dhidi ya harakati za kulinda haki za kibinadamu.
Raisi wa Uganda Yoweri Museveni alisema kuwa atapitisha sheria hiyo na itahusisha adhabu kali ikiwemo kifungo cha maisha kwa watakaogundulika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Lakini Obama alisema, Marekani imeiambia Uganda kuwa, kwa kuipitisha sheria hiyo uhusiano wa Marekani na uganda utapungua bila kufafanua kivipi.
Chanzo, VoA