Inaaminika kuwa kijana ni nguvu kazi imara katika jamii na ni tegemeo pia kwa jamii yake husika, kijana ndiye anayetegemewa kwa kila linalotokea kuwa mstali wa mbele kutafuta suluhisho.
Hivyo, kijana anashauriwa kuwa mstali wa mbele kujitoa kusaidia jamii yake pale inapokumbwa na majanga. Msaada huo unaweza kuwa wa uhamasishaji au wa kujitolea nguvu kazi.
Amka kijana, kuamka kwako kutasaidia kujenga jamii yenye vizazi vya watu wenye kujituma na maendeleo.