Imekuwa kawaida kwa majirani kugeuza nyumba za majirani zao ambazo bado zinaendelea kujengwa kama sehemu ya kutupa takataka badala ya kuzipeleka sehemu husika ya kuhifadhia takataka.
Ni tabia ambayo imeonekana kuwa sugu haswa katika jiji la Dar es Salaam bila kufahamu kuwa tabia hiyo inahatarisha afya zao dhidi ya magonjwa ya milipuko huku mmiliki wa nyumba hiyo akihitajika kutumia gharama za ziada kuondoa uchafu.
Amka jirani, hifadhi takataka sehemu husika iliyotengwa ili kujenga jamii safi na salama.