Thursday, 20 February 2014

KWA NINI FACEBOOK INAINUNUA WhatsApp KWA BEI KUBWA? msomaji wa vitendo blog fahamu zaidi hapa na vitendo.

Watumiaji wa WhatsApp ndio aina ya watumiaji ambao amtandao wa facebook inaowatafuta.

Watumiaji wa WhatsApp ni watumiaji walio na mwamko sana, wanatumiana picha zaidi ya milioni 600 ambazo ni zaidi ya facebook ambayo watumiaji wake utuma picha 500 kwa siku.

70% ya watumiaji wa whatsApp wanakuwa hewani ndani ya siku ukilinganisha na 62% ya watumiaji wa facebook kwa siku.

Watu dunia nzima wanatuma jumbe bilioni 19 kwa siku kupitia whatsApp, jumbe za sauti milioni 200 pamoja na video milioni 100 kwa siku.

Pia mtandao wa whatsApp una watumiaji wengi maeneo ya Ulaya, India pamoja na Latin America ambamo mtandao wa facebook unaanza kuimalisha mizizi yake.

Sifa hizi zote za whatApp ndizo ambazo facebook inazitaka ndio maana imekubali kugharamia bilioni 19 kuinyakua whatsApp.

Chanzo, CNN