Thursday, 20 February 2014

Msomaji wa vitendo blog, ebu angalia AMSHA AMSHA ya leo Feb, 20 na vitendo. Hii inakuhusu na ni muhimu sana kwako.

Inaaminika kuwa kuna baadhi ya maarifa ambayo mtu ana uwezo wa kujifunza bila hata kupitia darasani, ustaarabu ni moja ya maarifa ambayo hayahitaji darasa.

Mvuta sigara anashauriwa kuwa na ustaarabu wa kutambua kuwa uvutaji wa sigara kwenye kundi au mkusanyiko wa watu ni jambo lisilo la kistaarabu ambapo mtu asiyevuta anayeupata moshi anaathirika zaidi na inaleta kero pia.

Amka sasa, ili kuepusha matatizo yanayoweza kumpata anayepokea moshi wa sigara toka kwa mvutaji basi haina budi ustaarabu uzingatiwe.