Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu
uchi au kuhusika na vitendo
vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana
au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya
mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais
Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza
sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo vya
watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha
picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia
zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto
katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Kwenye picha ni wanawake kwenye maandamano kupinga sheria ya kuzuia nguo fupi
Chanzo, bbc swahili