Mhambuliaji wa zamani wa Simba Mganda, Emmanuel Okwia mbaye alikuwa tegemeo ndani ya kikosi hicho ameendelea kukosa namba ya kudumu katika kikosi chake cha Sonderjys kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.
Licha ya kwamba alikuwa lulu alipokuwa akiichezea Simba mshambuliaji huyo amekuwa si lolote nchini Denmark kiasi kwamba amejikuta mara kwa mara akianzia benchi.
Kinachomfanya Mganda huyo kujikuta benchi mara kwa mara ni kutokana na kukuta washambuliaji wazuri ndani ya kikosi hicho ambacho kinashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Bingwa newspaper