Sehemu yoyote inayokosa mawasiliano baina ya pande mbili zenye uhusiano basi lazima patokee kutoelewana.
Kutokuelewana huko kunakosababishwa na mawasiliano mabovu lazima kutasababisha matatizo na pande moja kati ya hizo mbili kuumia.
Kuumia huku kutasababishwa na utegemezi wa upande mmoja kwa mwenzie ambapo upande unaotegemewa utapuuzia kuimarisha uhusiano (mawasiliano) mzuri basi hili utokea.
Hali ya uhusiano huu naweza kuifananisha na ile iliyopo baina ya shirika la Tanesco wilayani Ruangwa mkoani Lindi na wateja wake.
Ni dhahili kuwa shirika hilo linakosa uhusiano mzuri na wateja wake kwa kushindwa kutoa taarifa muhimu kwa wateja wake.
Shirika linashindwa kutoa taarifa juu ya masuala kadhaa yanayoihusu Tanesco na wateja wao.
Inafahamika kuwa, mahali popote pale inapotokea itilafu ya umeme basi wateja wanapewa taarifa juu ya itilafu husika ili wapate kufahamu kwa nini huduma hiyo inakosekana
Si jambo la busara kwa shirika kukata umeme bila taarifa kuwa umeme unakatwa kuanzia saa fulani hadi saa fulani na ingekuwa busara kama ingekuwa inafanyika kinyume.
Kwenye hali kama hizi, taarifa kutoka Tanesco ni muhimu ili kuepusha matatizo yanaweza kujitokeza kwa wateja.
Idara ya mawasiliano Tanesco wilayani Ruangwa inapaswa iamke na kuhudumia wateja wake ipasavyo kwa kutoa huduma stahiki kwa wateja.
Lakini, kwa nini kuna wakati inashuhudiwa umeme ukikatwa na kurudishwa ndani ya muda mfupi?;
Kwa ufafanuzi wa swali hili ni kwamba umeme unakatwa na kurudishwa kana kwamba unachezewa na mtu fulani. Au kuna anayechezea?
Kitendo cha umeme kukatwa bila utaratibu maalumu ni hatari kwa watumiaji ambao wanaweza kuunguliwa na vifaa vyao.
Lakini ukataji huu usingekuwa hatari kama kitengo cha mawasiliano kingetoa taarifa kwa wateja wake ili kujiweka makini juu ya vombo vyao vya moto.
Badala ya kuwa hivyo, mambo huwa tofauti na ukosefu wa mawasiliano baina ya pande mbili hizi ikimaanisha Tanesco na wateja wao unapelekea kuumiza upande mmoja.
Upande huo unaoumia ni ule wa mteja ambaye anategemea kupokea kutoka Tanesco.
Kwa misingi hiyo sasa mteja huyu anayeachwa bila taarifa yoyote juu ya ratiba ya ukatikaji wa umeme ni dhahili kwamba lazima atapatwa na tatizo ambalo hatojua analitatuaje.