Monday, 31 March 2014

Tukio la kigaidi lililotokea kenya muda mfupi uliopita, sita wauawa. Mfuate vitendo kwa mengi zaidi.

Watu sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleigh, mjini
Nairobi.

Polisi wamesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika
mkahawa mdogo ulio karibu na kituo cha mabasi mtaani humo.

Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.

Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya
mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.

Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.

Inaarifiwa washambuliaji walitumia mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.