Saturday, 8 February 2014

SHULE DAR HATARI, WANAFUNZI NA WAALIMU WAKAA CHINI YA MITI.

Kukosekana kwa samani katika shule ya msingi Mtambani iliyopo wilayani kinondoni jijini Dar es salaam imepelekea wanafunzi wake kukaa chini, waalimu kutandika khanga na kukalia chini ya miti.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Emmanuel Munisi alisema shule hiyo ina ukosefu wa madawati, nusu ya wanafunzi wanakaa chini ya miti, hawana ofisi za kutosha na waalimu wao waliokosa nafasi wanakaa chini ya miti.

Aliongeza kwa kusema, tatizo hilo linawalazimisha kutandika khanga chini ya miti na kufanya kazi kwa sababu ya ukosefu wa meza za kufanyia kazi.

Hapo chini ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mtambani wakiwa shuleni.

Chanzo, NIPASHE.