Mwanasiasa mmoja nchini Colombia ametangaza kuifungia video ya mwanamuziki Shakira ijulikanayo kwa jina la "Can't Remember to Forget You" kwa kile anachodai kwenda kinyume na maadili ya Colombia.
Mwanasiasa huyo alisema kwamba kitendo cha Shakira kuonekana akivuta sigara, kuonekana baadhi ya viungo vya mwili wake na kuonekana akiwa kitandani pamoja na Rihanna wakishikana ni jambo ambalo ni kinyume cha sheria za vyombo vya habari nchini kwao.
Video hiyo aliyoshirikishwa Rihanna inayoonesha baadhi ya viungo vya miili yao,mwanasiasa huyo amesema inatishia uadilifu wa watoto na vijana nchini humo.
Chini ni moja kati ya picha za video hiyo.
Chanzo, CNN.