Thursday, 13 February 2014

MBARONI KWA KUDAIWA KUMUUA MWANAE KWA KUMBAMIZA KWENYE LAMI.

Onestory Mgaya (31), mkazi wa kijiji cha Madaba wilaya ya songea ametiwa mikononi mwa jeshi la polisi baada ya kumuua mtoto wake (7), Nesta Mgaya kwa kumbamiza kwenye lami akiwa amemshika miguu juu kichwa chini.

Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimenke alisema tukio hilo likitokea february 9 mwaka huu siku ambayo familia ya Mgaya walisafiri toka kijiji cha madaba kwenda kijiji cha Lilondo kusalimia wazazi.

Nsimenke aliendelea kusema,wakiwa njiani kurudi nyumbani, mkewe, Blesila Mponda alibaini kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao na kumwacha Mgaya barabarani na mtoto huyo ndipo Mgaya alipoanza kumbamiza kwenye lami barabarani akiwa amemshika miguu kichwa chini.

Nsimenke aliongeza kuwa, baada ya Mgaya kumbamiza alikimbilia polini baada ya raia waliokuwa karibu kukimbilia eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata.

Chanzo, Nipashe.