Wednesday, 25 May 2016

Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda apewa shavu hili na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU Dar es salaam
25 Mei, 2016

Furahia maisha blog