Wednesday, 25 May 2016

Usikate tamaa Wema sepetu, unakumbuka Sara wa Ibrahim alizaa akiwa mzee sana - Meneno ya shabiki mmoja wa Wema akimpa moyo juu ya kilio chake cha muda mrefu

Wema Sepetu ana kila kitu anachokitaka duniani, fedha, magari na vingine lakini amekosa kitu kimoja tu muhimu – mtoto.

Na Miss Tanzania huyo wa zamani anataka watu wajue kuwa suala la mtoto si kitu anachokichukulia poa hata kidogo. Muigizaji huyo alielezea hisia zake hizo kwa kupost picha akiwa na mama yake na kuandika:Ikosiku na mimi ntaitwa Mama.’Aliongeza emoji za mtu mwenye huzuni.

Miezi kadhaa iliyopita Wema na Idris walitangaza kutarajia kupata watoto mapacha lakini baadaye walitangaza kuwapoteza. Kwa muda mrefu Wema amekuwa muwazi kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba katika muda anaotaka kufanya hivyo.

Mashabiki wake wameendelea kumpamoyo na kumtaka asikate tamaa.

“Usikate tamaa @wemasepetu unakumbuka sara wa ibrahim alizaa akiwa mzee sana cha msingi endelea kumwomba mungu na jiweke karbu nae hakuna kinachoshindikana kwake,” ameandika shabiki mmoja.

Bongo5.com