Gunners wanataka kumpa Mesut Ozil dili jipya nono, na Arsene Wenger anatumai Mjerumani atakubali kubaki Emirates
Arsenal wanajipanga kumfanya MesutOzil kuwa mchezaji wao anayelipwa kuliko wote kwa kumpa mkataba mpya wenye thamani ya paundi 200,000 kwa wiki, kwa mujibu waThe Mirror.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amebakiwa na miaka miwili kwenye mkataba wake, lakini baada ya kuonyesha uwezo mkubwa Gunners wanataka kumtia kitanzi kwakumpa mkataba mpya.
Arsene Wenger ana imani mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid atakubali kujitia kitanzi kubaki Arsenal, baada ya kumpa mpya ulioambatana na bonasi za kutosha, mkataba utakaomwezesha kulipwa paundi 200,000 kila wiki - kiwango ambacho hakuna mchezaji wa Arsenalaliyewahi kukifikia.
Goal.com