Sunday, 15 May 2016

Mbakaji asababisha kifo cha kichanga

Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu mkazi wa kijiji cha Katenjele mjini Tunduma Mkoa wa Songwe (Shubati Kalinga) amefariki dunia baada ya kuangushwa akiwa amebebwa mgongoni na mama yake na mtu aliyetaka kumlazimisha mama wa mtoto huyo kufanya naye mapenzi kwa nguvu.

Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Dhahir Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki hii saa 11 alifajiri, ambapo mtu aliyefahamika kwa jina la Alex Mwema mkazi wa kijiji cha Mponela wilaya ya Mbozi alitenda kosa na kisha kutoroka mara baada ya tukio.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni kitendo cha mtuhumiwa huyo  kumlazimisha mama wa marehemu, Maria Mtindi kufanya naye mapenzi, kitendo kilichosababisha kumvuta na kusabisha mtoto kudondoka chini, ambapo alipata maumivu makali kichwani na kufariki dunia akiwa katika harakati za kupelekwa kituo cha afya cha mjini Tunduma kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Dhahir Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki hii saa 11 alifajiri.
Mwananchi