Sunday, 15 May 2016

Manchester United kuvamiwa tena

Manchester United imethibitisha kuhairisha mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Bournemouth kufuatia tishio la kiusalama lililogunduliwa uwanjani Old Trafford.

Dakika 20 kabla ya mchezo kuanza, mashabiki walianza kutolewa nje kuhofia tatizo ilo ambapo wanausalama waligundua kifaa kilichodhani kuwa ni bomu.

Baadae kidogo Man U ilitangaza kutokuwepo kwa mechi hiyo leo Jumapili ili kupisha ukaguzi wa kiusalama.

Polisi wanaotumia mbwa kugundua ualifu wapo kila kona ya uwanja wa Old traffod kujaribu kugundua chochote chenye madhara.