Tuesday, 17 May 2016

Makocha wanne wanaoweza kuchukua nafasi ya Van Gaal

Meneja wa Manchester United Louis Van Gaal alikuwa katika hali ngumu sana baada ya kupingwa na mashabiki, malegendi wa klabu na watangazaji ambao ni wachambuzi wa mambo ya soka. Meneja huyu Mholanzi alishindwa kuleta athari katika timu na klabu ingetarajiwa kuwa katika kiwango cha Barcelona, Bayern Munich na Real Madrid, na kwa upande mwingine alitolewa nje ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kupoteza dhidi yaWolfsburg vilisababisha kazi ya Van Gaal kuwa katika matata na wasiwasi. Hebu sasa tuangalie mameneja watano wanaoweza kuziba pengo katika Old Trafford ikiwa meneja huyu wa zamani wa Bayern Munich na Barcelona atafutwa kazi mwishoni mwa msimu huyu.

4.Diego Simeone
Katika miezi kadhaa ipitayo kulikuwa na ripoti kutoka Hispania zikisema kuwa meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone yaripotiwa kuwa aliamua kubadilisha ibara ya mkataba wake ili aweze kukubaliwa kukata kandarasi yake wakati wowote. Kwa mujibuwa taarifa za hivi punde, Simeone aliiambia klabu kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho katika Vicente Calderon.Manchester United inahitaji meneja wa kiwango hiki na kwa uhakika Mwajentina huyu anataka kuiondoka klabu katika kiangazi kijacho. Alifanya maajabu mnamo 2013 alipochapa Real Madrid na Barcelona na akashinda kombe la La Liga na Kombe la Mfalme (Copa del Rey). Walicheza pia fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidiya mahasimu wao Real Madrid na wakashindwa.

3. Mauricio Pochettino
Katika wiki ipitayo kulikuwa na ripoti zisemazo kuwa meneja legendi wa Manchester United Sir Alex Ferguson alikutana na meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino Mgahawani jijini London, kabla Red Devils washindwe 3-2 na West Ham United.Hapo awali Mkurugenzi huyu Ferguson alipata muda wa kumsifu Mwajentina huyu, akisema kwamba ndiye meneja bora katika Ligi Kuu ya Uingereza.Ingawaje Pochettino alisaini mkataba mpya na Spurs hivi punde, Sifa zake zilionekana na kuaminika kuwa ni ndiye meneja atakayeweza kuimarisha klabu hii ya Old Trafford.

2. Ryan Giggs
Meneja msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs alichukua madaraka ya ukufunzi wa klabu hii mnamo 2013 tangu David Moyes afutwe kazi. Louis van Gaal alipopewa kazi, alimpatia legendi huyu wa klabu nafasi ili aendelee kupata masomo ya kujizoeza kazi.Sasa mashabiki waamini kuwa Giggs amekwishakomaa vya kutosha na huu ndio wakati muafaka kuchukua timu kama meneja mkuu.Alitangaza hivi punde hisia zake huku akisema kuwa hakubaliani na maamuzi ya Louis van Gaal kama vile kumuachilia James Wilson aondoke klabu wakiwemowengine kama  Javier Hernandez, Danny Welbeck na Rafael da Silva.Mashabiki wadhani kuwa Giggs yaweza kurudisha sura Manchester United kama klabu ya soka kabla Louis van Gaal aiteketeze daima.

1. Jose Mourinho
Meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho ni mmoja miongoni mwa mameneja waliofanikiwa zaidi katika ulimwengu wa soka. Alishinda Ligi ya Mabingwa na vikombe vya ligi kadhaa katika klabu tofauti barani Ulaya. Alitwaa taji la Ligi Kuu ya England Capital One Cup msimu upitao akiwa na Chelsea.Kwa muda mrefu alikuwa na hamu ya kumrithi Sir Alex Ferguson lakini ndoto hazikufanikiwa kutokana na sababu zisizojulikana hadi sasa, na badala yake wamiliki wa United walimpendelea David Moyes. Kwa kipindi hiki hawangekuwa na uchaguzi mwingine isipokuwa kumpa ajiraMreno huyu.

Sokkaa