Tuesday, 17 May 2016

Anthony martial kurithi nafasi ya Ibrahimovic zlatan PSG

Paris Saint-Germain waripotiwa kwamba wanapanga kumrudisha Anthony Martial nchini Ufaransa katika kiangazi hiki kama mrithi wa Zlatan Ibrahimovic, ripoti kutoka L’Equipe kupitia Sportsmole.

Mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Manchester United kiangazi kipitacho Monaco dili yenye thamani ya £36m ambayo inaweza kuendelezwa hadi £58m.

Mfaransa wa kimataifa alikuwa mshambuliaji kabambe katika msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo aliweza kufunga mabao 17 katika mashindano yote chini ya umenejimenti wa Louis van Gaal