Monday, 23 May 2016

Ipitie ripoti kuhusu nchi ya China kujihusisha na uuzaji wa nyama ya binadamu Afrika

Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama yang'ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China aliyesema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.Balozi wa China nchini Zambia,YangYouming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.

''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyamaya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.''Hii ni dhulma ya makusudi ambayohaiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.