Kufuatia mechi ya fainali ya mabingwa Ulaya kati ya hawa wenyeji wa Madrid Atletico na Real madrid kila mtu anawaza yake juu ya nani ataibuka mshindi.
Kila mmoja anatabiri yake kuhusu idadi ya magori yatakayofungwa na timu ipi itafunga mangapi na ipi itashinda mangapi.
Katika kulielezea hili, mshambuliaji matata wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amekuja na utabiri wake wa timu ipi itaibuka mshindi na kwa kuonesha yeye ana uwakika na timu anayosema itashinda yani ameipa na idadi ya magori pia.
Katika picha hapo chini Aubameyang anaonekana kuipa nafasi Real Madrid. Ameipa ushindi wa magori 3-2 dhidi ya maasimu wao Atletico.
Wacha tusubiri tuone kama huu utabiri unaotolewa utakuja kutimia hiyo tarehe 29 ndani ya San Siro.