Cristiano Ronaldo yuko katika hali ya mashaka kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mahasimu wa jadi Atletico Madrid siku ya Jumamosi, baadaya kuumia pajani mwishoni mwakikao cha mazoezi Jumanne asubuhi.
Mreno wa kimataifa amepata kuumia vikali alipogongana na golikipa Kiko Casilla baada ya kusukumwa na Dani Carvajal.
Nyota huyu apata maumivu wakati kunabaki na siku nne ili timu hizi zipepetane katika fainali ya Ligi ya Mabingwa jijini Milan kwenye uwanja wa San Siro.