Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo anaamini kuwa uamisho uliofanywa na Manchester united wa kumsainisha Jose Mourinho ni mzuri.
Ronaldo anaamini kuwa Manchester United imepoteza utambukisho wake tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson lakini anaamini ujio wa Mourinho ni mzuri kwa klabu.
Ronaldo amekaa Old Trafford kuanzia mwaka 2003-2009 kabla ya kujiunga na Real Madrid ambayo iliongozwa na Jose kwa misimu mitatu.
“Nadhani ni vizuri endapo kama ndicho Manchester walichokuwa wanakitaka,” Ronaldo aliiambia La Sexta's 'Jugones'TV show.
“Natumai Manchester United itarudi katika hali yake ya kawaida kwa sababu ni klabu inayovutia sana lakini miaka ya hivi karibuni imepotea kidogo.
“Na inaniumiza sana kuiona Man U katika hali hii kwa sababu ndio klabu ninayoibeba moyoni mwangu.” Ronaldo alisema.