Michezo 8 ya kuhitimisha hatua ya makundi kwa michuano ya klabu bigwa barani ulaya ilipigwa jana usiku.
Ambapo timu kumi na sita zimefuzu kuingia raundi ya pili ya mtoano michuano hii.
Manchester City wakiwa katika uwanja wa Stadio Olimpico walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2 -0 dhidi ya wenyeji Roma na kufanikiwa kuingia kumi na sita bora kwa kushika nafasi ya pili kwenye kundi E.
Chelsea wakiwatungua Sporting Lisbon kwa goli 3-1 Mabigwa wa Ufaransa PSG wakakubali kichapo cha goli 3-1toka kwa Barcelona, CSKA Moscow wakalala kwa kuchapwa goli 3-0 na bayern munich, FC Porto wakatoka sare ya 1-1 na Shakhtar Donetsk,Ajax wakipata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Apoel Nicosia, Schalke 04 akimchapa 1-0Maribor huku Athletic Bilbao wakiwabanjua BATE Borisov kwa goli 2-0.
Droo ya upangwaji ratiba kwa michezo ya kumi na sita bora itapangwa jumatatu Desemba 15 hatua ya mtoano itaendelea tena februari.
Huku ikishuhudiwa mabigwa mara tano wa michuano hii Liverpool, pamoja na Olympiakos, Zenit St Petersburg, Anderlecht, Roma, Ajax, Sporting Lisbon, Athletic Bilbao wamejikuta wakiangukia kwenye ligi ya Europa baada ya kushindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano.