Sunday, 16 November 2014

Umeipata hii ya mlipuko wa mafua ya ndege Uingereza?

Mlipuko wa mafua ya ndege umethibitishwa katika shamba moja la kuzalishia bata mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa.

Wizara ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini (Defra) imesema hatari kwa afya ya umma ni ndogo sana. Ndege wasiohitajika wanaondolewa kutoka eneo hilo na eneo la kuwatenga limeandaliwa.

Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa Defra.

Kirusi hicho husambaa kati ya ndege na katika matukio ya nadra, kinaweza kuwaathiri binadamu.

Eneo la kuwatenga ndege lililopo kuzunguka shamba hilo litazuia ndege na kinyesi cha ndege ndani au nje ya eneo hilo.Ndege wote pia watatengwa.

Mlipuko wa ugonjwa hatari wa mafua ya ndege uligundulika Jumapili katika shamba moja nchini Uholanzi.

Tukio hili huko Yorkshire ni la kwanza nchini Uingereza tangu mwaka 2008, wakati ulipozuka. Mafua ya ndege daima yamekuwa yakidhibitiwa kikamilifu nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara amesema: "tumethibitisha tukio la mafua ya ndege katika shamba la kuzalishia bata huko Yorkshire - afya za watu haziko katika hatari na hakuna hatari katika vyakula. "Tunachukua hatua za dharura katika kukabiliana na janga hili ambazo zinahusisha eneo la kilomita 10 na kuwaondoa ndege wote katika shamba kuzuia uwezekano wa kusambaa kwa mambukizi. Uchunguzi wa kina kuhusu ugonjwa huo unaendelea.

Tuna rekodi nzuri ya udhibiti na utokomezaji wa milipuko ya ugonjwa wa ndege iliyowahi kutokea siku za nyuma nchini Uingereza."

Via bbcswahili