Kukomoana kwa kuchapisha picha za Utupu za mtu binafsi, bila yeye
mwenyewe kujua, imekuwa ni suala kuu duniani katika miaka ya hivi karibuni.
Nchini Uganda picha za utupu za
mwanamuziki Desire Luzinda
zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na magazetini.
Inasemekana mpenzi wake wa zamani ndiye aliyechapisha picha hizo kwa lengo la kumuadhibu mwanamuziki huyo.
Waziri wa maadili nchini humo anataka mwanamuzki huyo akamatwe kwa kupigacpicha za utupu.