Wanasayansi wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema dawa zinaonesha kuwa
salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua virusi hivyo.
Watu 20 waliojitolea kutoka nchini
Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.