Jamaa aliyekuwa anaendesha baiskeli kwa mkono mmoja kutokana na ulemavu ajikuta akitozwa faini ya paundi kadhaa kwa kuendesha baiskeli kwa mkono mmoja.
Bogdan Ionescu, alisimamishwa na askali wa barabarani nchini Ujerumani na kutozwa faini hiyo kwa kuwa pia baiskeli hiyo ilikuwa na breki ya mkono wa kulia tu.
Lakini baada ya kuichunguza baiskeli hiyo waligundua kuwa Bogdan Ionescu aliruhusiwa kisheria kuendesha baiskeli kwa mkono mmoja kwa kuwa breki nyingine ilikuwa inaendeshwa kutumia mguu.
Msamaha ulitolewa kwa Bogdan Ionescu toka kwa askali hao baada ya kugundua walimkosea.