Tuesday, 6 May 2014

Teknologia hii ni ulinzi tosha dhidi ya wezi, mwizi ajikamatisha bila kujitambua

Simu ya mkononi iliyokuwa imeibwa, ilituma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo
kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.

Polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo ambayo ni aina ya HTC, iliyoibwa kutoka kwenye koti la
mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.

Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza namba ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.

Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanamume huyo alipojaribu
kuingiza namba hiyo bila kufanikiwa.

Barua pepe ya mwanafunzi huyo ilituma ujumbe kwa polisi kuwaarifu kuhusu wizi huo.

Mwanaume aliyejipiga picha bila yeye kujua