Msichana wa miaka10 kutoka shule ya msingi ya Oklahoma amedaiwa amebakwa na mvulana wa miaka 8 akisaidiwa na dada yake ndani ya choo ya shuleni kwao.
Mama wa msichana aliyebakwa alisema kuwa alikuwa akimsubiri mwanae nje ya shule ndipo baadae mtoto huyo alipotoka nje huku analia na alipomuuliza kimetokea nini mtoto alisema "mama, nimeguswa chini huku."
Msichana aliyebakwa alisema kuwa, alikuwa chooni ndipo mvulana aliyembaka akaingia akiwa na dada yake wa miaka 10 na kumfanyia kitu mbaya.
Mama wa msichana huyo alisema kuwa, msichana wake alipiga mayowe ya msaada lakini mvulana mbakaji na dada yake walimnyamazisha kwa kitisho kuwa wangempiga kama angeendelea kupiga kelele.
Baada ya msichana huyo kufanyiwa uchunguzi hospitalini, madaktari walisema kuwa ana majelaa ya kawaida.
Mama wa msichana huyo alisema kuwa hawalaumu watoto ila anawalaumu waalimu ambao hawakuwa makini na watoto hao.
Maafisa kwenye shule hiyo wanafanya uchunguzi kamili juu ya tukio hilo.
Mama wa msichana ambaye hakutaka kujulikana. Via Dailymail