Thursday, 8 May 2014

Foleni Dar inaaribu ndoa

Kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Chilaga Isaack mkazi wa Yombo Dar es salaam, amejikuta akiiweka ndoa yake katika hali ya hatari baada ya kuchelewa kurudi nyumbani toka kazini kwa sababu ya foleni kubwa ya magari barabarani.

Isaack alisema kuwa aliporudi nyumbani majira ya saa 4 usiku nyumbani alimkuta mchumba wake amekasirika na alianza kumuuliza maswali ambayo yalimweka kijana huyo kwenye wakati mgumu na wakati huo dada huyo akidai kurudishwa kwao.

"Unajua huyu mchumba wangu anadhani kwamba mimi nilikuwa na mwanamke sehemu fulani wakati haiko hivyo bali ni foleni tu barabarani iliyonifanya nichelewe kurudi", alijitetea Isaack.

Tatizo la foleni jijini Dar linazidi kuwa kubwa na kutengeneza usugu jambo linalosababisha raia wengi wa Dar kupatwa na matatizo mengi mno.

Tatizo hili la foleni bado utatuzi wake unaonekana kusuasua licha ya wahusika kuonekana wakikaza msuri na kuahidi kulipatia ufumbuzi bila mafanikio yoyote.

Baadhi ya barabara za jijini Dar zikiwa zinamsongamano mkubwa