Monday, 12 May 2014

Ajinyonga kwa kukatazwa kutumia facebook

UK
Msichana mmoja wa miaka,13, amejitia kitanzi baada ya mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Aditi Gupta kupigwa marufuku na mama yake asitumie mtandao facebook.

Aditi Gupta alichukizwa sana na uamizi huo wa mama yake wa kumpiga mkwara kutumia facebook kwa muda usiojulikana na kuamua kujitundika chumbani kwake.

Mrs Gupta kabla ya kwenda kazini alimtaka Aditi aifunge akaunti yake ya facebook na pindi atakaporudi akute tayari ameshafanya hivyo ila baada ya kurudi toka kazini Mrs Gupta alimkuta mwanae ameshajinyonga.

Sababu kuu iliyomfanya Mrs Gupta limkataza mwanae ni kwa sababu umri wake bado ulikuwa hauruhusu kujiingiza kwenye utumizi wa facebook.

Via Dailymail